Friday

Mume wangu namtaka na Bf namtaka-Ushauri

"Habari dada Dinah,
Mimi ni dada wa miaka 29, ambaye niliolewa miaka 7 iliyopita pia kwa kipindi chote niliwahi kushika ujauzito wa miezi 7 kisha mimba ilitoka. Hadi hivi leo yapata miaka mitano sijawahi tena kupata ujauzito.

Mume wangu ni Mzungu na ni mtu wa makamo ambaye kanipita zaidi ya miaka 29. Dada na wadau wengine nakiri nilijiwahisha kuolewa kwa tamaa ya pesa na maisha bora kutoka kwa Mzungu huyo.


Ni kweli vipesa vya kubadilishia nguo, mboga hazinipigi chenga. Miaka yote sita tuliishi Tz lakini sasa tumeamua kuwa huku ughaibuni. Dada tatizo langu la kutoshika mimba lilinichanganya mpaka nikaunda urafiki wa chinichini(siri) na kijana mwenzangu Mtanzania ambaye yupo bongo, niliona ngoja nijaribu huku nione kama mimi ndio ninatatizio au mume wangu.


Dada tumetombana wee siku za hatari najiachi sijaona dalili yeyote ya mimba. Pamoja na kujaribu urafiki na kijana mwenzangu tumechonga mzinga kwani urafiki wetu ni wa miaka 3 sasa, mwenzangu yeye yupo single.

Sasa dada si unajua mapenzi ya kijana kwa kijana ni raha tupu ukimpata awezae? dada sio siri huyu boyfriend ananifikisha kunako halafu ni very hadsome......mwangu ana V shape,ananipeti vilivyo, ingawa kipato chake si kama changu.

So ndugu zanguni juzi juzi nimeenda Bongo mwenyewe bila ma husband, basi boyfriend akaja nipokea tulieenda kulala hotelini siku hiyo sikutaka kwenda kwangu mbezi, tulikuwa tumemisiana kichizi.


Ila kufika usiku mpenzi wangu huyo alinieleza kuwa eti anataka kuoa, ametafutiwa mke Mombasa na bibi yake, pia ndugu wanamkera kuwa lazima aoe. Sio siri mimi nina moyo mwepezi ikaniuma basi nililia ingawa nimeolewa.


Akasema sasa kama wewe upo Ulaya unakaa miezi 3 ndio unakuja Bongo, tena unarudi Ulaya lipi bora mim ikuoa au kukaa na kufuta machangudoa? Pia nilisha mwahidi kuwa ningemsaidia juu chini naye awe huku Ughaibuni?


Hivi ndugu tarehe 24 Januari ndio Ndoa. mimi nampenda, pia nina wivu nae sana, Pia ameniomba pesa ya mchango wa harusi, nikimuliza anadai ooh hata kama naoa fanya juu chini unilete Ulaya na huyu mke ataenda kukaa kwao Mombasa.


Anaendelea ooh yote umeyataka wewe kwani siku zote hizo ningekuwa nawe Ulaya mke ningepewa saa ngapi. Na yeye pia anaonekana upendo nami bado. Jamani namzimia, anasifa nizihitajizo za kuitwa mwanume, anajua jinsi ya kuniandaa kuliko mume wangu.


Jamani pia nawahasa watu wasomao haya umri katika mapenzi ni kitu kizuri. Wazee bwana akifanya ni kimoja kwa week, au mbili, sometime ukimkalia utafikiri atakufia, akitomba kimoja atahema kama anakata roho.


Ndugu naombeni ushauri wenu, pia nimekiri kusaliti ndoa yangu najua ni dhambi, mume wangu namtaka handsomeboy namtaka niko njia panda dada yenu.

asanteni nawatakia HAPPY NEW YEAR:"

Jawabu: Habari ni njema tu Mdada, shukrani kwa kuniandikia, nitarudi baada ya muda mfupi kutoa maelezo yangu ambayo kwa namna moja au nyingine yatakusaidia ukiongezea na yale yaliyokwisha elezwa na wasomaji wangu.

Ni kweli kabisa watu wengi tu wanafunga ndoa kwa sababu fulani na sio mapenzi kama ambavyo baadhi yetu tunaamini, ni sehemu ndogo sana ya watu ambao wanafunga ndoa kwa sababu ya kupendana na kutaka kuishi kwa shinda na raha maisha yao yote. Umenifurahisha kwa kuwa muwazi kuelezea hali halisi na kwanini ulifunga ndoa na Mumeo huyo.

Ndoa bila mapenzi-Uamuzi wa kuolewa ili kuishi maisha fulani au kupata kitu fulani(makaratasi) sio wa ajabu kwa wanawake na wanaume wengi wa Kiafrika, lakini tofauti ni kuwa wengi wao hujitoa mapema mara tu baada ya ile "plan" kukamilika na kuachana Wazungu wa kisha kwenda kuendeleza mapenzi ya kweli huko waendako.....kila mtu nahitaji kupenda nakupendwa, maisha yangekuwa jehanam kama kusingekuwa kuna mapenzi baina ya watu wawili.


Kitendo unachokifanya nje ya ndoa yako sio kizuri na ni ukatili wa hali ya juu kwa mume wako. Ikiwa uliolewa kwa ajili ya kuishi maisha ya hali ya juu (ilikuwa mission) sasa ulitakiwa kuwa mbunifu na kufanya miradi ili kuchuma vya kutosha kisha ujitoe kwenye ndoa ambayo haina mapenzi ya dhati na imejaa uongo kitu kinachokufanya usiwe na raha wala amani.


Baada ya kujitoa (kuachana) ndio ungeenda kutafuta mapenzi na mtu mwanaume mwingine ukiwa huru na usingeumiza hisia za mumeo ambae mpaka sasa hajui kuwa anachangia mwili wako na mwanaume mwingine!......jaribu kujigeuzia angekuwa yeye mumeo anafanya hivyo na mwanamke mwingine ungejisikiaje?


Nilichogundua hapa ni kuwa ulikuwa na hisia za kimapenzi na mumeo na ndio maana mpaka leo bado uko nae, ila tatizo ni wewe na mumeo, hamlizungumzii hili suala la kujaribu njia tofauti ili mfanikiwe kupata mtoto.

Kutokana na tofauti kubwa kiumri huyo bwana (mumeo) anaweza akawa na huruma sana kwako na kuku-treat kama mtoto wake zaidi kuliko mpenzi, hali inayoweza kusababisha ashindwe kukumbushia suala hilo la kujaribu uzazi tena akijua ile mimba iliyoharibika imekuathiri Kisaikolojia (which ni kweli na nina amini kabisa kuwa kichwani hakuko sawa) na asingependa kukuumiza.

Mimba-Ikiwa ulishika mimba na ikatoka baada ya miezi saba (alikuwa mtoto mkubwa kabisa, tunasema "mtoto alifia tumboni") ni wazi kuwa mumeo hana matatizo yeyote, inawezekana wewe ndio unamatatizo yanayohusiana na viungo vyako vya uzazi kwa ndani.


Badala ya kwenda kutembea ovyo na mtu mwingine ulipaswa kutulia na kutafakari maisha yako ya nyuma na kutafuta nini hasa kinaweza kuwa sababu ya mimba (mtoto) kuharibika ndani ya miezi saba, sio hivyo tu bali ulitakiwa kuwa karibu na Madaktari wa magonjwa na kike na wale wanaojihusisha na masuala ya mimba na uzazi ili wakuchunguze na kuona kama kuna tatizo lolote lilijitokeza baada ya "mimba" kutoka, huenda ulihitaji kusafishwa mara kwa mara kwa mara...tafadhali fanya mpango ukamuone Daktari wako haraka iwezekanavyo.


Mapenzi na kjn-Linapokuja suala la mapenzi hakuna umri ni utundu, ujanja, kujali na kujituma kwa mtu umpendae. Kwa vile wewe upo kwenye ndoa bila kuwa na mapenzi na mumeo ndio maana ukahisi hivyo ulivyohisi. Kutokana na sifa ulizomiminia ni wazi kuwa unapenda huyo kijana na uko comfy kuwa nae karibu.

Nyumba ndogo kuoa-Kutokana na "hadithi" yote huyu kijana anachotaka kutoka kwako ni pesa au kurushwa/vutwa Ughaibuni na ile kujituma kwake ktk kufanya mapenzi ni moja ya mbinu zake ili avutwe na wewe haraka, lakini wewe ulichelewa kufanikisha hilo akabidi aje na "plan B" .

Baada ya kugundua hakuna juhudi zozote za kuharakisha na kumrekebishia mamabo ya kusafiri, ndio kakujia na "plan B" ambayo alijua wazi kuwa inakuumiza na itakufanya ufanye haraka kuweka mambo sawa ili aje kuishi huko uliko wewe.

Ktk hali halisi na maisha tunayoishi hivi sasa kijana kutafutiwa mke na bibi yake au hata baba yake haipo sana, japokuwa kuna ndugu na jamaa kutaka sana mtu afunge ndoa lakini bado unapewa nafasi ya kuchagua.....huwezi ukaenda kufunga ndoa na mtu kwa vile Bibi kamleta! Anachotaka hapa ni wewe kuwahisha mipango aondoke Bongo.

Huyu kijana angekuwa na mapenzi ya kweli kwako na sio mapenzi ya Ughaibuni angekushauri tangu mwanzo kuwa uachane na huyo Mzee (since u r not in love) ili yeye afunge ndoa na wewe na muende kuishi wote huko majuu.....hapa utaona wazi nini anachokitaka "out of relationship".


Kwa mwanaume, ngono haina maana sana kwao kama sisi wanawake, anaweza kuwa na uhusiano na wewe wa kingono na kuifanya vema kabisa lakini hisia zake za kimapenzi hazipo kwako. Atafanya kila awezalo ili kupata akitakacho.....in ur case ni kubebwa nje ya nchi.

Nini cha kufanya-Achana nae, yaani uhusiano wenu uwe umekufa kuanzia hivi sasa na mchango wa harusi yake usitoe. Najua itakuwa ngumu sana kwavile kijana anakaa Bongo na wewe unaishi huko uishiko. Kata mawasiliano (block mail Add na namba yake). Kuachana na mtu uliejenga hisia za kimapenzi juu yake sio rahisi lakini inafikia wakati inabidi tu uachane nae na kuendelea na maisha yako.

Umekaa kwenye ndoa bila mapenzi kwa muda mrefu sana, karibu miaka nane! Hiyo ni adhabu tayari kwenu nyote, kama nilivyosema hapo awali. Ikiwa umechuma vya kutosha, unamakaratasi ya nchi husika na bado unahisi kutompenda huyo "babu" basi anza mbele kwa faida yake na yako.

Tafuta Wanasheria wanaojihusisha na Talaka na watakupa ushauri mzuri na kutaliki mumeo usiempenda kama ifuatavyo.....lakini hakikisha unabakiza urafiki kwa maana kuwa usioachane na kibabu cha watu kwa fujo na vita na kuua urafiki, keep the friendship na kuwa pake kwa ajili yake akihitaji msaada ili kuonyesha shukrani kwa ulichovuna kutokana na yeye kukuoa wewe miaka nane iliyopita.


Bada ya hapo utakuwa huru ku-date mwanaume kijana yeyote utakaemdondokea na yeye kukufia. Maish aya kimapenzi sio rahisi na mara zote huwa tunafanya makosa ambayo tuki-share kwa uwazi na watu wengine kwa namna moja au nyingine tunasaidia watu wengine wasifanye makosa kama yale tuliyofanya sisi.

Psst-Siku hizi hata wanaume wamekuwa "wachunaji" a.k.a wizi, inaweza ikawa sio kujihusisha kimapenzi na wewe mwanamke bali hata kutaka mfanye biashara ambayo haipo.

Natumai maelezo yangu ukichanganya na ya wachangiaji utakuwa umepata mwanga wa nini cha kufanya. Nakutakia kila la kheri kwenye uamuzi utakao uchukua.

No comments:

Pages