Sunday

Ushuhuda! Katangaza ndoa lakini....Ushauri!

"Dada dinah pole sana kwa kazi za kuelimisha jamii. Mimi ni msichana wa miaka 24 ,nina tatizo ambalo naomba msaada wako pamoja na wadau wengine tena naomba kama inawezekana unipe favour unisaidie angalau ndani ya wiki hii ili nisije nikajiharibia.


Dada tatizo langu ni hili; mimi nina mchumba ambaye tunategemea kufunga ndoa mwezi wa tano mchumba wangu ambaye kwa kweli nampenda sana yeye anakipato kidogo ukilinganisha na mimi, lakini nimejitahidi kumuonesha kua fedha wala dhahabu haviwezi kuleta furaha ya moyo.

Sasa juzi alinifuata na kuniomba nimsaidie kulipa mahari jamani kweli nilisikitika alivyo kujana kuniambia ''dia kweli nakupenda toka moyoni na napenda ndoa yetu iwe hata kesho tatizo linakuja kua hela zina nipungukia na natakiwa mwezi wa pili nipeleke mahari nisaidie mpenzi nimekwama '' ukizingatia kua huo mwezi wa pili ndio anatakiwa aende ili akapewe tarehe ya ndoa.

Kusema kweli hela anayoipata ni ndogo ukilinganisha na kile anachodaiwa, sasa dada naogopa kumsaidia japo naumia sana, naogopa baadae kwenye ndoa asije akaniletea dharau kua hatamahari ulijilipia mwenyewe.


Nisaidieni kua nimsaidie au nizibe masikio japo ni mambo mengi tuna saidiana ila hili nimeliona ni kubwa. Nitashukuru kupata ushauri wenu ilinikaufanyie kazi .


USHUHUDA: Dada mimi nilisoma Makala yako inayo husu jinsi yakumfanya mwanaume atangaze ndoa, kweli nilifanya hivyo na nikashangaa siku tatu baada ya kumfanyia vibweka nikashangaa anakuja nakuomba tena kwa magoti ''Dia naommba unisikilize shida yangu '' nikamuinua eeeh sema shida gani ya kunipigia magoti ? nataka tufunge ndoa yani tena mwakani sitaki hata mwezi wa sita ufike .

Nikauliza kulikoni mpenzi, nikasikia ooh nimeamua tu. Nikahoji utaamuaje fasta hivyo ? nikasikia "duh hayo maswali mengi sana ina maanisha hutaki ?" nikasema kimoyomoyo mambo ya dada Dinah hayo , nikasikia dia nataka nifaidi kwa karibu sasa najua nikibung'aa nitakuta mwana siwangu.


Kuuanzia pale wivu ulizidi nikashangaa ananisindikiza kila mahali ukaribu ulizidi sana wakati mwingine naambiwa kabisa mama unanitia wivu. Samahani kwa mlolongo wa maneno. Nilikua najaribu kutoa ushuhuda ."

Jawabu-Hongera sana kwa kufanikiwa kumfanya atangaze ndoa, unajua kuna wanaume wengine wanakuwa na wewe kwenye uhusiano kwa muda mrefu bila kuonyesha nia ya kutaka kuwa na wewe daima (Ndoa), sio kuwa hataki bali anadhani bado anamuda wa kusubiri sasa hilo likitokea basi ndio wewe mwanamke unapaswa kumsaidia kwa kumfanyia mambo niliyoelezea ambayo wewe uliyafuata na yametimia.


Ushirikiano-Ni moja kati ya nguzo tano za kuboresha uhusiano wowote wa kimapenzi, tunapozungumzia kushirikiana na kufanya mambo pamoja kwa faina yenu nyote wawili hatuzungumzii kwenye kuwa pamoja katika kufanya maamuzi au kufanya mapenzi tu bali hata kwenye suala zima la kiuchumi.


Ninyi ni wapenzi na uhusiano wenu ni mzuri na baada ya muda mfupi mtakwenda kula kiapo cha kuishi maisha yenu yote kama mke na mume. Hili likitokea ni wazi kuwa kutakuwa na suala la kusaidiana ili kufanya maisha yenu ya ndoa yawe mazuri na kuishi vile mpendavyo na sio kwa shida kuu.


Kutokana na maelezo yako unaonyesha ni binti mwenye kuthamini mwanaume na haujaegemea sana kwenye suala la Usawa ambao mimi huwa naona ni ujeuri ambao wanawake wengi wanaubeba kwa kisingizio cha "Usawa" na ndio maana mpenzi wako akawa huru kuja moja moja kwako na kuomba msaada, katika hali halisi alipaswa kwenda kuomba/kopa rafiki zake au hata baba yake.


Mahari-Haya ni malipo yanayotolewa na mwanaume ili kuruhusiwa kuoa binti husika, matumizi na maana ya "malipo" haya ni tofauti na inategemea na Mila za wahusika. Mf-Ninakotoka mimi mahali sio ya wazazi, wajomba na shangazi bali ni yako wewe binti.


Ikipokelewa kama ni mifugo au pesa basi baada ya muda unakabidhiwa kwa maana kuwa unahitaji kitu cha kuanzia maishani wewe na mume wako. Mahari hiyo haiesabiki kuwa inatoka kwa kijana anaetaka kuoa bali inatokwa upande wa pili yaani familia ya mumeo, sasa binti hapa anaweza kupewa nafasi ya kutaja kiasi cha "malipo" anachotaka kutoka upande wa pili na mara nyingi Mahari hiyo hutumika kufanya maandalizi ya sherehe ya ndoa na sio kuanzishiwa biashara (hakuna kulipana ikiwa ndoa itaharibika).


Vilevile binti anaweza kuamua mahari ilipwe kwa mafungu (taratibu) au asipokee kabisa na hii inategemeana na uwezo wa familia ya mpenzi wake ambayo kwa wakati huu atakuwa anaijua vema.


Lakini Mila nyingi huwa na malipo ya awali ambayo ndio muhimu "kimila" ( na sio pesa nyingi, zaidi ni kununua vifaa/vitu fulani fulani kwa wanafamilia bibi, mkwe sijui mkaza mjomba n.k) kabla Mahari haijalipwa, hayo yakikamilishwa mipango ya ndoa inaanza mara moja na Mahari inaweza kulipwa baadae hata baada ya kufunga ndoa.


Kasumba-Suala la "ndio maana ukajilipoa mahali" lisikusumbue kichwa, ni kasumba tu ya wanawake wajinga wajinga ambao wanaamini kuwa ni lazima kuolewa na mwanaume mwenye "mahela" na wanaangalia zaidi kiasi gani cha pesa as for Mahari mwanamke mwenzao kalipiwa.......lakini katika hali halisi ulipiwe elfu 20 au milioni 50 bado utahitaji mapenzi na mambo mengine mengi ambayo hayahusishi pesa, ili kuifanya ndoa yako iwe nzuri, yenye afya, furaha na amani hapo baadae.


Nini cha kufanya-Mchumba wako kasema (kama ulivyoandika) "Dia kweli nakupenda toka moyoni napenda ndoa yetu iwe hata kesho tatizo linakuja kuwa hela zinanipungukia natakiwa mwezi wa pili nipeleke Mahari nisaidie mpenzi nimekwama".


Huyu bwana (kutokana na nukuu hiyo hapo juu) anaomba kuongezewa pesa ili a-top up kile kidogo alichonacho ndani ya muda aliopewa na sio kukuomba wewe mpenzi wake ujilipie Mahari yote, kwa maana nyingine, inawezekana kabisa ikawa sio msaada wa pesa anaotaka kutoka kwako bali ni wewe kuzungumza na familia yako kumpa muda zaidi wa kukusanya pesa ili kukamilisha mambo.


Kama kweli mnapenda na nia yenu ni kuishi kwa shida na raha maisha yenu yote yaliyobaki basi msaidie kwa kuongezea kile kidogo alichonacho. Huitaji kumwambia mtu yeyote kuwa umemuongezea mchumba senti ili akamilishe mahari on time. Chukulia kuwa mmeamua kuchanga kufanya jambo muhimu kwa ajili ya maisha yenu kama vile kununua kiwanja na kujenga nyumba pamoja.

Kila la kheri ktk kukamilisha shughuli za ndoa. Mungu akujaalie.

No comments:

Pages