Thursday

Hivi huyu ananipenda au Mchunaji?-Ushauri!

"Hi Dinah mdogowangu hujambo?
Naomba msaada wa ushauri kwa wanablog wenzangu. Mie ni mama mkubwa kiasi kwa umri, Nilikua na mwanaume tuliokua dini tofauti na tumeachana kwa miaka miwili sasa.


Kuna kijana ambae nimemzidi kwa takriban miaka miwili alivyosikia kama niaeachiaka tu, hapo hapo akaniambia yeye ananitaka na dakika hiyohiyo akaniambia kama niko tayari basi anaweza kufunga ndoa hata kesho, nilibaki nashangaa kwa nini haraka?


Mie sikumpa jibu la ndio wala hapana lakini nikabaki kumuambia labda ananijoke asingeweza kunioa kwa kua mie mkubwa kwake. Hali yangu kiuchumi na hata assets sio mbaya sana, Yule kijana ana kazi , ila kiuchumi nimemzidi ana mke na watoto watatu, ni muislam ndoa ya pili inaruhusiwa.


Alikua anamwamko sana wa kwenda kuongeza shule (degree ya pili) lakini hakua na sponsor na mwajiri alimkatalia ruhusa na akataka kuacha kazi, nilimshauri asiache ambembeleze mwajiri ruhusa. Sasa nikajiuliza ana mapenzi huyu au anataka kunituma nimsomeshe?


Baada ya mawasiliano, tukapoteana kwa kipindi kirefu kidogo kwa kuwa nilikua nje ya nchi. Tumeonana mwezi wa kwanza ki-accidental, ile mada imeanza tena, Na sasa ameshapata admission IFM hana sponsor, mimi niko nje ya nchi tena ila yeye anasisitiza anataka kuowa hata kwa remote, (kwa waislamu inaruhusika).


Najaribu kumsihi kwamba sasa hivituwasiliane tu na tuchunguzane, lakini yeye ameng'ang'ania antaka jawabu la kukubaliwa tuoane au laa ajikate. Hakuwa moyoni mwangu sana lakini nilikua nahisi with time hasa ukizingatia umri wangu naweza kumpenda.


Lakini ameng'angania ananipenda na anataka jawabu. Kwa tabia kama mme ndani simjui vizuri, nilijaribu kumuuliza kijana anaefanya nae kazi akaniambia kazini hayuko-organized na yuko hash, kwa nyumbani sijuiiii.

Wana blog naomba mnisaidie mawazo huyu kijana ananipenda kweli, au anataka kunitumia? lugha zake za kusisitiza hilo suala sikuzipenda sana kwani kunasiku ashaniambia ukinikataa mimi hutapata tena mtu kama mimi au hutapata mtu atakae kupenda kama mimi, au kwanini hujiulizi ni nini nilikupendea nisipende wanawake wenzio.nk.

Naomba ushauri jamani, ananipenda huyu? nimkubali? nimemwambia tusubiri kwa kua sipo nchini hadi november tuyazungumze yeye kagoma. Ushauri jamani hili jamaa linataka nini?"

Jawabu:Mimi sijambo Dada'ngu, habari za wakti kama huu mpendwa!
Huyo isije kuwa ni mmoja kati ya wale "wezi watupu", dada unajua siku hizi hata wanaume tena walio na familia zao(wake na watoto) wanachuna wanawake ambao mambo yao ni safi kiuchumi?.

Tena siku hizi nasikia wanawake walio nje ya Bongo au wenye kujiweza ndio wanaoibiwa kweli kweli, unaweza teremka pale Yapoti (airport) ukapokelwa na vijana/babaz watanashati wakitoa "offers" tofauti tofauti za ndoa hihihihihi.....turudi kwenye somo.


Kwenye maelezo yako tangu mwanzo mpaka mwisho hakuna mahali umeelezea hisia zako juu ya huyo kijana. Huyu kijana ni kweli anataka mdhamini kwa ajili ya masomo yake ya juu na ndio maana akakurukia mara tu alipogundua kuwa wewe na mumeo/mpenzi mmeachana.


Inawezekana kabisa kutokana na "kasumba" alidhani wewe utakuwa "desparate" kuwa na mwanaume au kuolewa kama inavyoaminika kwa wanaume wengi kuwa unapokuwa mdada mkubwa na kisha kuachika basi unakuwa huna "bahati", hivyo pamoja na kuwa ni mdogo kwako aliona utamkubali tu bila mizengwe.


Kwa upande wa pili huenda kijana kweli anakupenda, lakini je wewe unampenda? Tangu umetoka kwenye uhusiano mwingine ambao naamini ulikuwa wa muda mrefu na "serious" ni wazi unahitaji muda kuchuja hisia zako ili kuwa na uhakika vilevile kuwa tayari kujiingiza kwenye uhusiano mpya wa kawaida wa kimapenzi acha ndoa.


Kutokana na maisha ya sasa hakuna kitu kinaitwa kuchunguzana ili kufunga ndoa(ilikuwa miaka hiyo), siku hizi kupendana kwanza, ndio majuana taratibu na kuchunguzana na kuerekebisha kama inawezekana alafu unamalizai nakufanya maamuzi ya busara baada ya kugundua kasoro zake na yeye kugundua zako na kisha kujitoa mhanga na kukubali kuishi maisha yako yote (kufunga ndoa) bila kuzijali kasoro zake na utakachokifanya ni kumpenda mwenzio kila siku kama ndio mmeonana wiki iliyopita.....vinginevyo ndoa itakuwa ndoano.


Sasa, suala hapa sio kama yeye ni mchunaji au lah, kitu muhimu hapa ni wewe na hisia zako juu yake. Je unahisi kumpenda? kama sio je unadhani unaweza kurafikiana nae kikawaida tu? Vilevile unadhani siku moja unaweza kupendana nae na kuwa zaidi yamarafiki wa kawaida?

Nakuja....

No comments:

Pages