Sunday

Nilitoka na mume wake,nimesaidia wamerudiana lakini....

"Hey Dinah, natumai kuwa wewe ni mzima kabisa. Mie nina changamoto ambayo naamini kabisa wanablog wenzangu wanaweza kunisaidia kwa ushauri.

Nina BF ambaye nimekuwa naye kwa miaka mitatu sasa, kwa vigezo nilivyonavyo ni kwamba nampenda sasa kabla sijakutana naye sikuwahi kufikiri wala kutamani kuolewa. Isipokuwa niliwahi kuwa na BF ambaye tulikuwa marafiki wa kawaida kwa muda mrefu kabla ya kuamua kungonoana then we parted ways.

Mapenzi yetu yalikolea na kuwa matamu zaidi automatically tukajikuta tunakaa pamoja. Kwa kweli sikuwahi kusikia raha ya kuwepo dunia kama wakati huo. Lakini wakati sisi tukiendelea kufaidi maisha kwa kiwango hicho BF wangu alikuwa ametengana na mke wake kwa mifarakano ambayo wenyewe wanaijua na kwa muda mrefu wamekuwa wakikaa mikoa tofauti mpaka sasa.


Nadhani mke wake alikuwa akitufuatilia na kujua kuwa tupo pamoja. Asili ya kazi zangu ni safari, hivyo katika safari zangu nilikwenda Mkoa ambao mkewe anaishi. Nikakutana naye akanifanyia bifu baadae tukapata audience akaniuliza kama nipo na mumewe mie nikatoa nje kwani niliogopa mkono maana nilimwona mshari kama nini.


Kwa bahati mbaya au nzuri nikaenda tena katika Mkoa ule tukaonana akanihadithia mambo mengi kuhusu mume wake ambaye mimi ni BF wangu. Alinieleza walianzia mbali katika maisha na kwamba sasa wamefika pazuri mume wake ndio anamfanyia hivyo.


Nilimwuliza kama mumewe anatunza watoto wao 2 akasema ndiyo lakini anataka arudi kwake kwani anampenda sana. Nilimwonea huruma na ikanigusa sana kwa sababu mimi ndiye ninayesababisha hivyo.


Niliporudi home nilimketisha BF nikamwambia situation na kwamba uamuzi wangu ni kwamba kwa kuwa sina mpango wa kuolewa basi we could be together while she is with his wife and everything will be ok.


To my surprise alikataa katakata kwamba yeye hamtaki na wala hana mpango wa kumrudia. Mimi nilihisi kwamba inawezekana anahisi namtega but I was very sincere. Siku zikapita na mimi huruma ikaendelea kunishika lakini mume wa mtu nampenda.


Tukawa tunapanga mikakati mingi na mke wake ili nimsaidie mumewe arudi kwake kumbuka kwamba nimekataa katakata kwamba mimi sipo na mume wake. Kwa bahati mbaya sana alikuja mkoa tunaoishi kwa majukumu ya kifamilia (msiba).


Kama baba wa watoto iliwajibika kumfariji na nadhani hapo ndipo walipo ombana radhi na kusameheana , wakaanza upya. Mimi pia nipo pembeni nafurahia mafanikio yao. Mke wake akaendelea kunisisitiza nimsaidie ampate mwanamke aliyemkamata mume wake. Kwa mara ya kwanza niliona kuwa ananitega lakini moyoni nikasema mtego huo hauwezi kunikamata.


Naomba nikufahamishe kwamba aliponiuliza mara ya kwanza nilikataa kushirikiana na mumewe lakini nilikiri kumfahamu na kwamba huwa tunawasiliana isipokuwa ni nyanja za kazi tu. Nilipoona anazidi kusisitiza nimsaidie nikamua kufikia maamuzi magumu sana ya kumwacha mpenzi wangu huyo.


Ilikuwa ngumu sana kwani nampenda sana huyu mwanaume. Nilijaribu kumwambia kwa lugha ya taratibu na upole sana lakini hakuwa tayari kabisa. Nilimwambia nafanya hivyo kwa ajili yake na mke wake. Bado akakataa.


Nilimtoa nyumbani kwa nguvu na kwa ugomvi mkubwa sana. Ilikuwa vibaya kwa sababu tulikuwa tukiishi nyumbani kwangu. Aliona kama nimemnyanyapaa. Baadaye alifanikiwa kuondoka na kurudi kwake. Hata hivyo alikuwa anakuja nyumbani kwangu mara nyingi tu.


Baada ya muda mrefu wa mawasiliano ya mbali hivyo akaanza kukata mawasiliano kwa muda mrefu kama wiki mbili tatu hivi simsikii. Akiibuka anasema atakuja nyumbani anataka kungonoka. Tukingonoka anapotoea tena kwa muda wa mwezi or so na akirudi anataka kungonoka.


Hiyo tabia ikanichosha nikaamua kumwambia kwamba ilipofika panatosha kwa sababu naona kama ananifanyia mzaha na kutaka kuniumiza roho. Yeye akasema kwamba nilimuumiza sana kwa kumfukuza nyumbani kwangu na kwamba jeraha nililosababisha litachukua muda kupona.

Mimi nimechoshwa na hiyo tabia na kila ninapojaribu kumwacha nashindwa kwani akitokea nasahau kwamba nilitaka kumwacha tunaendekeza libeneke.

Wanawake wenzangu nisaidieni lakini pia wanaume naomba ushauri kwani tabia zenu zinafanana.
Kim from Atown"

Jawabu:Hi Kim, hapa kila kitu kiko sawia kabisa. Kwanza napenda kukupa pongezi kwa kutokuwa mbinafsi na kumsaidia mwanamke mwenzio kurudiana na mume wake. Hongera sana kwa hilo.


Ni kawaida kwa wake na waume ktk umri fulani kutojiona au kufikiria kama sio kutamani kuolewa au hata kuzaa (muda ukifika utalifikiria hilo na kutenda kama ifuatavyo), natambua uamuzi wako wa "kutojikita" kwenye ndoa ulikufanya uone kawaida kutoka na mwanaume yeyote utakae mpenda bila kujali kaoa na familia au la, nafahamu uamuzi wako ulikupa hali ya kujiamini sana kama mwanamke kitu ambacho ni kizuri...i mean kujiamini.


Lakini katika hali halisi no matter how unajiamini na kujitegemea usithubutu kutoka na mume wa mtu kwa kudhania kuwa hutoruhusu akuoe au kumuacha mkewe kwa ajili yako......kwani kwa kufanya hivyo sio tu utakuwa unaumiza mwanamke mwenzio bali pia utakuwa unaharibu mpangilio mzima wa maisha ya mtoto au watoto waliozaliwa kwenye ndoa hiyo na vilevile kufanya watu ktk jamii kutothamini ndoa(kitendo chako kinatoa ujumbe kuwa huthamini ndoa za watu).


Kutokana na sehemu ya maelezo yako inaelekea huyu bwana pamoja na matatizo mengine ya kindoa kama vile kuzozana mara kwa mara kitu kinachoweza kusababisha asipate ngono na mapenzi ya kutosha kutoka kwa mkewe.


Huyu bwana sio tu alikuwa akihitaji hifadhi kutoka kwako ili apumzike kiakili (kutokana na matatizo ya kindoa) bali na ngono pia. Unajua, linapokuja suala la ngono, akili kutulia na kuwa "comfy", hakuna maswali ya kipuuzi-puuzi, lawama za kizembe na malalamiko ya ajabu-ajabu kama sio kusingiziwa, mwanaume wanaweza kuhamia na kusahau familia yake kama unavyo "blink" vifuniko vya macho yako......bila shaka umeshuhudia hilo na unauzoefu mzuri tu.


Kuachana na mtu unaempenda ni ngumu sana na ndio maana huwa nawashauri "wateja wangu" kama kweli wanania ya kufanya hivyo lakini upande wa pili bado unasumbua kama huyo Ex bf wako ni kukata mawasiliano kwa kubadilisha nambari za simu na anuani ya makazi. Vinginevyo kila mkionana utahisi kutaka kuwa karibu nae na kufanya chochote na hivyo uhusiano wenu utakuwa ule wa on and off kwa vile wewe bado unampenda na yeye bado anapata ngono tamu na ya bure kutoka kwako.


Lakini kwa vile mkewe anamtafuta "mwizi wake" ambae ndio wewe lakini yeye hajui kuwa wewe uliyesababisha mumewe arudi nyumbani ndio "adui" ni vema kuachana kabisa na huyo bwana kwani huwezi kujua huyo Mdada anataka kumfanya nini huyo aliyemlia mumewe.....well huenda anataka tu kujua nini ulikuwa ukimfanyia mumewe ili na yeye afanye (fanya utafiti ujue anataka nini hasa kutoka kwa mwizi wake kwanza hehehehe unaweza kutolewa macho kama sio roho.......mtu chake atii).

Sasa mimi nakushauri utumie nguvu (kibali cha Polisi) ili kuzua huyo bwana asije tena kwako, kwa kufanya hivyo itasaidia wewe na yeye kuepuka "ngono chafu" na mume wa mtu. Natambua kuwa unampenda huyo mume wa mtu lakini kumbuka sio wako na kamwe hawezi kuwa wako.

Pamoja na uamuzi wako wa kuwa mwenyewe for life haina maana basi utembee na mwanaume hata kama ni mume wa mtu, jaribu kuwa mchunguzi unapotaka kuanzisha uhusiano ili usirudie kosa. Hakikisha unamfahamu mhusika kabla hujaji-comminte kwake kama mpenzi, hakikisha unakujua kwake, anaishi na nani n.k.

Wapo wanaume wengi tu ambao hawana wake kwa vile hawako tayari kuoa kuoa kwa mara ya pili baada ya Talaka au wake zao wamefariki dunia, nadhani wanaume wa namna hiyo wanakufaa zaidi na mtakuwa compartible in a way.

Kila la kheri.

No comments:

Pages