Thursday

Hivi huwa tunajiandaa tunapoanza familia?



Nimeshuhudia sehemu kuwa ya watu hapa Duniani huamua kuwa na familia (kuzaa) kwa kushitukizwa (bila kuwa tayari). Kwa vile mimi ni m-bongo na nina uzoefu au nawajua wabongo basi nitaegemea huko kwa m-bongo halisi.


Sina hakika kama ni ubinafsi au ile kasumba ya kipuuzi kwamba ukiachia mimba basi Mpenzi hakuachi, pia inawezekana kabisa kuwa ni uzembe wa mtoa mbegu (mwanaume).


Kisheria (as far as I remember) umri wa kushiriki ngono/funga ndoa ni 18+ japo kuwa bibi yangu aliolewa akiwa na miaka 15 akaja kuzaa mtoto wa kwanza akiwa na miaka 20 ila kwa karne hiyo kulikuwa na sababu ya kuolewa ktk umri mdogo ambazo sote natumaini tunazijua.

Sasa ndugu zangu mnapo amua kupeana mimba huwa mnakuwa mmejiandaa baada ya kung'amua faida, majukumu, matatizo, mabadiliko ya kiakili na kimwili (mwanamke)?

Je, huwa mnakuwa na uhakika na uamuzi wenu au mmoja anaamua ili kumridhisha mwenzie au jamii inayomzunguuka? au hutokea tu kwa "bahati mbaya"?
Huwa nasikitika sana ninapo ona binti au kijana huyu mdogo ambae katoka kwa wazazi (bado mtoto) kisha akawa mzazi na yeye kwamba hajui tofauti au mabadiliko ya mwili wake kutoka Utoto, Ujana na kufikia Utu uzima na anapofikia umri mkubwa (utu uzima) anakuwa amejichokea(kazeeka).

Kijana/binti huyu hajafaidi ujana wake....sio kufanya ngono ovyo bali kufanya yale mambo ambayo vijana tunapenda kuyafanya bila kuwa na hofu "mtoto" atakula nini kesho, sijui anaumwa, amekua unahitaji vivazi vipya, siku gani ni clinic, je mpenzi wako ana-cheat n.k., kujua tofauti ya kupenda (bila ngono), n.k.


Ongezea basi uonavyo wewe (bila ku-attack mtu) mimi nasikia usingizi, swaumu kali hapa!

Nakuja......

No comments:

Pages