Sunday

Kukata kiuno...."basic"


Nakumbuka nilipokuwa mdogo kabla hata sijaanza shule kila jioni tulikuwa tukikusanywa nakuimbiwa nyimbo fulani za Mwinamila na kulazimika kukata viuno, usipokata kiuno hakuna kuadithiwa hadithi usiku chini ya mbala mwezi (aah utoto raha sana).

Nilipokuwa binti mkubwa nikawa naambiwa kuwa usipofanya mzoenzi ya kukata kiuno utakuja kupata taabu pale nitakapo olewa ikiwana maana kwamba unazungusha kiuno kwa ajili ya bwana.

Lakani mimi leo nawapa "basic" ya mauno sio kwa ajili ya kuwanufaisha wanaume zenu bali kuwasaidia ninyi kufurahia wakati wa kufanya mapenzi/ngono.


Kwanza anza na kulizoesha tumbolako kabla hujahamia kiunoni au kwenye hips. Sote tunatambua kuwa tumbo ni moja ya sehemu inavutia kama ilivyo makalio, miguu n.k. hasa kama tumbo hilo ni kama langu (dogo )hahahaha.



Haya tuanze zoezi basi ili usije shitua utumbona makorokoro mengine pale utakapo kurupuka na kuanza kuzunguusha kiuno chako.



1-Simama wima(ukiwa uchi mbele ya kioo ndio it'll work better), weka mikono yako hapo tumboni alafu sukuma tumbo lako mbele (litunishe) baki hivyo kwa muda kisha lirudishe kwa ndani na ubaki tena hivyo kwa muda. Rudia kufanya hivyo mara nyingi uwezavyo na kumbuka kubana pumzi huku mdomo ukiwa wazi (itasaidia kukaza misuli ya tumbo pia), kubadilisha mirindimo (polepole, haraka, chap-chap, kugandisha n.k) mpaka utakapo hizi tumbo lako linatetema/tikisika (yaani vibrating).

Msingi wa kukata kiuno

Kama nilivyosema awali, simama wima najishike kiunoni(kuhu na huku) kisha peleka sehemu ya kiuno ya kulia upande wa kulia, sehemu ya mbele ipeleke mbele uwezavyo(nina maana ile pelvis tu sio tumbo na kila kitu) alafu baada ya hapo peleke sehemu yako ya kiuno ya kushoto-kushoto, kisha peleka seheumu yako ya mbele nyuma hali itakayofanya matako yako yabinuke/jitokeze kwa nyuma.....nyoosha magoti kisha rudi kulia(ulipoanzia).



Fuata hatua hizo kwa mara nyingine tena ambazo ni simama wima-kulia-mbele-kushoto-nyuma kulia x 20 na kuendelea inategemea zaidi na bidii yako.



Baada ya kuzoea hatua hizo hapo ndio unapotakiwa ku-create movements na mirindimo yako kivyako. Mfano lala chali, kifudifudi(lalia tumbo), ubavu, chutama, piga magoti n.k kisha nenda kulia-mbele-kushoto-nyuma-kulia mpaka kiuno kizoee......hey alafu usisahau ukiwa ndani ya "game" kukilazimisha mpaka kitakapo kubali/zoea.


Kidokezo: Zoezi zuri la kukata kino ni kulala kifudifudi(kulalia tumbo) kisha kukizunguusha (hapa usipokuwa mwangalifu unaweza ku-cum via kisimi kwa vile unatua unakisugua kiaina sio mbaya ni njia moja wapo ya kujipunguzia stress sio hahahahaha).


Haya Zeze endeleza somo bidada.


Nikirudi nitakueleza tofauti za ukati kiuno na faida zake.

No comments:

Pages