Monday

Wanaume, tupendeni kwa vitendo!


Wakati wa kunanihii si mara zote huwa penzi......

Kwenye moja ya makala zangu kuna mshirika (Moses) aligusia mahitaji ya wanawake na wanaume ktk mahusiano ya kimapenzi(nitalizungumzia hilo ktk siku zijazo).
Leo napenda kugusia kidogo kuhusu hitaji moja mbalo sote tunahitaji lakini tuna feli (fail) kulitekeleza, hitaji hilo ni “Affection” ukilitekeleza ni kuwa “affectionate” kwa mwenza wako…………Kiswahili chake ndio nini?
Tumeshuhudia mahusiano mengi ya kimapenzi kuanzia baba na mama, ndugu, jamaa na marafiki wakipendana au kuwa pamoja kama wapenzi, lakini ni mara chache sana utawaona hawa wapenzi wakionyeshana kuwa wanapendana kwamba sio “affectionate".
Ni kweli kuwa unampenda mwenzi na unamjulisha unampenda kwa kumwambia, lakini kumbuka kuwa penzi ni hisia ulizo nazo wewe juu yake. Unahisi kabisa bila yeye wewe ni hamna kitu hapa Duniani lakini yeye haoni hilo unless ufanye kwa vitendo yaani uonyeshe unampenda mwenzio.
Huenda ni kutokana na tamaduni au mila na desturi kwamba hupaswi kufanya mambo Fulani ukiwa nje ya chumba/nyumba, lakini kuna baadhi ya watu hata wakiwa mahali peke yao kama wapenzi huwa hakuna kutekeleza hilo hitaji kitu ambacho mwenza wako ataona kama vile humpendi au humjali na uko nae kama msaidizi (ATM,mpishi,usafi n.k) au mtu wa kukuburudisha kwa kutumia mwili wake.

Kuwa “affectionate” kwa mpenzi wako huitaji kumkumbatia na kumlamba/busu mbele ya kadamnasi bali unaweza kumshika mkono,kutembea nae ubavu to ubavu (sio baba mbele mama nyuma na furushi lake kichwani) vilevile unaweza msaidia furushi ukiweza unambebea hata mkoba wake n.k..

Kwa sasa naishia hapa, nitarudi baada ya masaa machache kumalizia, karibu

No comments:

Pages