Friday

Kumbe mpenzi ni Kaka...nimerudi tena-Ushauri!


"Habari dada dinah mimi niyule dada ambaye sikujua kuwa mpenzi wangu ni kaka tatizo lingine limejitokeza, nilikuwa naenda kuoga na simu yangu niliiacha kitandani mara baada ya kutoka kuoga nikakuta dada yangu ameshikilia simu yangu.



Dada akaniambia/uliza "yaani we unatembea na Kaka" (tumuite Beka) akaanza kunitukana kwa kuniita "malaya mkubwa wewe hata baba yako mzazi utatembea nae na kuanzia sasa hivi nitakuwa na mchunga hata mume wangu".




Dada dinah nifanyaje? naumia kwa kutukanwa na dada yangu hasa kuniita hivyo, nisaidieni jamani? je nimuache huyo mtoto wa binamu wa mama yangu ambae ni mpenzi wanfu au nifanyaje? "


Jawabu: Pole sana kwa tatizo lingine lililojotokeza hivi sasa, Kuitwa Malaya mbona ni kawaida tu, wala huna haja ya kumia au kuwa na huzuni kutokana na kitu kidogo namna hiyo.



Lakini jamani, inakuwaje mtu mwingine achukue simu yako ya mkononi na kusoma msg au hata kupokea simu bila ruhusa yako? Hicho ni kitu binfasi na kinaweza kuwa na mambo mengi binafsi ambayo hayapaswi kuonwa, sikiwa, somwa na mtu mwingine unless ni mpenzi wako.



Baada ya ushauri uliotolewa hapa umeufanyia kazi au unaendelea kuufanyia kazi? Kama ungeufanyia kazi mapema hili suala la dada'ko kukutukana lisingekuwepo au lisingejitokeza. Mpenzi "Kaka" anasema nini kuhusu uhusiano wenu?



Wakati mwingine mwanadamu unapaswa kuwa a little bit selfish na kutojali kwa sana hawa ndugu ambao hivi sasa kila mtu anaendesha maisha yake kivyake. Dada yako anamaisha yake na mume wake na anapaswa ku-focus huko, Mama yako anamaisha yake na mume wake ambae ni baba'ko na anapaswa ku-focus huko na wewe una maisha yako kama binti mdogo lakini unataka kuwa na maisha yako kama wao kwa kuungana na mtu mwingine ambae mnapendana na atakuwa baba wa watoto wako na unapaswa ku-focus huko.



Pamoja na kusema hivyo sina maana kuwa uwadharau, hapana. Endelea kuwaheshimu, sikiliza ushauri wao na fanya maamuzi ya kuyafanyia kazi au kuyaacha pale pale kama yalivyowakilishwa kwako.



Ulisema kuwa wewe na mpenzi wako mnakwenda kufunga ndoa(Ikiwa nakumbuka vema, nitaangalia). Kama kweli mnapendana na mnania moja na huyo Ndugu yako wa jina (sio wa damu) basi kuweni "serious" na fungeni ndoa (sio lazima iwe kubwa na kushirikisha kila mtu, mnaweza kufanya ya kiserikali ili wewe na yeye kuishi pamoja na kihalali kama mke na mume) ili kumaliza kesi.




Fanya uamuzi wa busara kwa kuzingatia nani ni muhimu kwenye maisha yako kama mwanamke, mama ambae anamaisha yake? dada ambae anamaisha yake? au Mume wako ambae mnapendana na mnakwenda kuwa na maisha yenu pamoja?



Vinginevyo matatizo yatazidi kujitokeza juu ya matatizo mengine ambayo ukiyafuatilia kwa karibu utagundua ni kupotezeana mida tu.


Kila lililo jema!

No comments:

Pages