Wednesday

Nampenda rafiki wa X je nimkubali?-Ushauri.

"Hello Dinah kwanza pole na kazi,
Mimi ni msicha mwenye umri wa miaka 26, mwanafunzi wa moja kati ya vyuo hapa Tanzania. Shosti nahitaji sana ushauri maana maji yamenifika shingoni. Nilikuwa na Boyfriend kwa muda mrefu lakini kwa bahati mbaya mimi nikapata shule mbali kidogo na mkoa ninaoishi.



Boyfriend wangu alifurahi lakini nahisi haikua furaha ya kweli kwani baada ya kuondoka na kukaa miezi sita hapo shuleni tabia yake ilibadilika nikimpigia simu anashindwa kuongea nikimwambia nimemiss ananijibu kana kwamba kuna mtu anamuogopa.


Baada ya mwezi mmoja baadae alinitumia message na kuniambia ana msichana mwingine kwasababu hajaweza kuvumilia, I was so frustrared baada ya kusikia hivyo kwani nilikua nampenda lakini baadae nilifikiria nakugundua hakuna umuhimu wa kuendelea nae nikamjibu kama ameamua hivyo ni sawa.


Tatizo linakuja huyo boyfriend wangu alieniacha ana rafiki yake ambaye nasoma nae chuo na anajua uhusiano tuliokua nao, ila baada ya kujua kuwa rafiki yake siko nae tena ameanza kunitaka na mimi nampenda sana na napenda awe boyfriend wangu kwani nae hana msichana kwa sasa je Dinah NIMKUBALI huyu mwanaume because I real need a boyfriend au itakua vibaya kwasabau ni rafiki wa my X boyfriend?"


Jawabu:Wanawake wa magharibi wanaamini kuwa sio vema kutoka na mwanaume kutoka kwenye mzunguuko wa rafiki zake na ni mwiko kabisa kutoka na Ex mpenzi wa rafiki yako wa kike, lakini ndio wanaongoza sio kutembea nao bali ni kuwaiba kabisa!. Sasa kuna faida gani kujiwekea miiko wakati wanashindwa kuitekeleza?



Huyu bwana hana undugu na Rafiki yake, hivyo kama mnapendana kweli na mnania moja ya kuwa kwenye uhusiano go for it!


Lakini kama huna uhakika na hisia zako za kimapenzi lakini kwa vile unahitaji kuwa nae (kama ulivyosema) "I really need a boyfriend" basi ningekushauri usimkubali kwa sasa na badala yake usubiri kwanza mpaka utakapo kuwa "in love" ili uhusiano uwe extra special n avilevile usije ukaumizwa hisia tena.




Take it slow ili kujenga hisia halisi na za kweli za kimapenzi na kumbuka tu kuwa " You can never need a boyfriend, (they come and go)....you need Education (you will have it for the rest of your life).....we only want them.

Nakutakia kila lililojema.

No comments:

Pages