Sunday

Kuzuia mimba kiasili-Ushauri





"Samahani dinah mie kidogo niko nje ya mada ningeomba sana unifahamishe jinsi ya kuzuia mimba kwa njia ya kalenda kwani nimechoka kutumia midonge jamani tafadhali nifahamishe mpenzi ndugu yangu.




Yaani huwezi amini kitendo cha kuwa na mpenzi wangu kinanifanya niumwe kwa kufikiria mimba tu. Nimekua muoga mchezo nautaka ila tatizo kuingia kwa mimba hivyo basi nakuomba chonde chonde unifafanulie jinsi ya kuzuia kwa kutumia tarehe tafadhali naomba."


Jawabu: Asante kwa uvumilivu wako pia kwa ushirikiano wa kuuliza swali lako mahali hapa. Njia ya asili ya kuzuia mimba ni mbinu pekee ambayo wanamama wa miaka ile kabla ya madawa ya kisasa(kizungu) kugunduliwa. Njia hii inauhakika wa asilimia 96-mpaka 98 kama zilivyo njia nyingine za kuzuia mimba kama vile vidonge, sindano, patch, Coil. Njia nyingine asilia ni kumwaga nje (withdrawn), lakini hii unahitaji zaidi ushirikaino wa mpenzi wako, mawasiliano wakati wa tendo kwani akijisahau au kuchelewa ujue kitu na box.


Mipira (Condoms) ndio kinga pekee inayozuia mimba na magonjwa yote ya ngono kwa asilimia 99 na ile moja iliyobaki ni kwa ajili ya sababu za kisheria kulinda Makampuni incase mtu akatumia vibaya na kushika mimba au gonjwa la zinaa. Vilevile Kinga hii (Condom) ndio pekee ambayo ham-badilishi mwanamke kihomono au kimaumbile.



Njia ya asili ya kuzuia mimba hutumiwa na wanawake ambao kwa namna moja au nyingine hawataki kutumia madawa ya kisasa ili kuepuka mabadiliko ya miili yao kama vile kunenepa, kutokwa na majimaji ukeni na pia kuna tetesi kuwa yanaongeza uwezekano kwa mwanamke kupata Saratani ya Kizazi na Matiti.


Kuzuia mimba kwa kutumia tarehe inauhakika ikiwa mzunguuko wako ni uleule na sio mrefu (siku 32-35) wala mfupi (siku 18-24) bali ni ule wa kawaida ambao ni siku 28. Ili kutumia mtindo/mbinu hii ya kuzuia mimba unapaswa kuanza kuhesabu siku zako sasa na fuatilia kwa karibu mzunguuko wako na kuhakikisha kuwa una siku 28 sio chini wala juu ya hapo, kwa kawaida unaaza akufuatilia kwa miezi mitatu hadi sita (kama umewahi kutumia madawa ya kuzuia mimba) kabla hujaanza kuitumia njia hii.


Namna ya kuhesabu nitumiayo mimi-Ili kuwa na uhakika na urefu au ufupi wa mzunguuko wako unapaswa kuhesabu siku ya kwanza utakayo ona damu mpaka utakapo ona damu ya mwezi utakao fuata.

Mfn; leo tarehe 12 mwezi wa kumi na moja ndio umeanza hedhi basi hedhi ya mwezi ujao itakuwa tarehe 10 mwezi wa kumi na mbili.....hii ni kama mzunguuko wako usiobadilika (sio mrefu au mfupi) ambao ni siku ishirini na nane tu.



Siku ya kwanza ya hedhi mpaka siku ya tisa ni salama na huwezi kushika mimba, baada ya hapo mpaka siku ya kumi na nne (yai linapevuka) unakuwa hatarini, siku ya kumi na saba mpaka siku ya ishirini na mbili unakuwa salama tena mpaka siku ya ishirini na tatu mpaka ishirini na saba (yai pevu linashuka) hatarini lakini ile ya ishirini na nane siku ya hedhi nyingine unakuwa salama tena......comfusing ei?




Ili kuwa na uhakika kuwa uko kwenye mstari kuliko kuegemea kwenye tarehe tu unatakiwa kujua mabadiliko ya mwili wako. Unapokuwa hatarini kushika mimba mara nyingi utahisi nyege zaidi n avilevile utoko wako utabadilika na kuwa mlaini zaidi (kama lotion) na wakati mwingine utahisi ute unatoka (ule kama udenda/mlenda)....ukiona hivyo hakikisha unatumia Condom vinginevyo utashika mimba.
Unapokuwa salama mara nyingi hamu ya kungonoka inakuwa haipo sana unless "uchokozwe", vilevile utoko wako unakuwa mzito (kama cream/mafuta mazito)na mweupe sana yaani hata wakati wa kujiswafi inakuwa taabu na inaweza kukuchukua muda mrefu zaidi. Hali ikiwa hivi ujue uko salama kungonoka bila kinga ya kuzuia mimba.

Kila la kheri!

No comments:

Pages