Tuesday

Miaka 5 na mume wa mtu, Familia hamtaki-Ushauri.

"Habari yako da Dinah !!!!

Mi msichana mwenye umri wa miaka 29, sasa nimekuwa na uhusiano na mwanaume wa mtu takriban miaka mitano sasa na kipindi chote tulichowahi kukaa ananijali sana na kunitimizia mahitaji yote ninayohitaji ikiwa ni pamoja na mapenzi ya dhati mpaka ikafika kipindi mkewe akajua lakini baadae mwenyewe akasalimu amri na kutuacha tuendelee na penzi letu.


Sasa dada yangu kinachoniumiza kichwa familia yangu haitaki kumsikia kabisa huyu kaka na tumeshapanga mipango mingi ya kimaisha so niko kwenye "dilema" najiuliza nianzie wapi kwani nilishawahi kumgusia hiyo ishu tukagombana sana na akaishia kusema atakuwa mgeni wa nani kwa sababu mkewe ashamtenga hawajagongonoka miaka yote 5 wala kulala kitanda kimoja toka alipogungua mumewe ana uhusiano nje.


Na mimi pia kwa sasa naona ni mda wangu wa kumpata mume awe wangu peke yangu naomba ushauri wako dada nifanyeje na wadau wa blog hii nisaidieni kwasababu toka nimekuwa na huyu jamaa hajawahi kujitokeza mtu hata kusema nakupenda ya unafiki.


Kazi njema dada Dinah tunashukuru sana kutuelimisha kupita hii blog yako Mungu akubariki."

Jawabu: Aisee nimeshituka lakini nimefurahishwa na uwazi wako, ndio nia na madhumuni ya D'hicious watu kuwa wazi kwani sote tunajua haya mambo yapo na ya natokea, hapa tunasaidiana na kujifunza namna ya kukabiliana nayo kama sio kuyazuia yasitokee kabisa. Safi sana dada.

Unajua kuna mambo mengine unatakiwa kujigeuzia kibao kwanza upate picha ya itakavyokuwa kabla hujaamua kutenda......ingekuwa wewe ndio mkewe na akaamua kutoka na mwanamke mwingine ungefanya nini? ungejisikiaje?


Alafu mwenyewe hapo mwisho umesema kuwa unadhani kuwa sasa ni muda wako wa kuwa na mume wako peke yako, kutokana na maelezo yako ni wazi kuwa unaamini kuwa kila mke anapaswa kuwa na mume wake peke yake.


Lakini umesahau kuwa huyo mpenzi wako sio wako peke yako na hata akikuoa hatokuwa wako peke yako, hajawahi kuwa wako peke yako na basi hivyo hatokuwa wako peke yako.


Kutembea na Mume wa mtu ni kosa, hata siku moja usijaribu kulala na mume wa mwenzio ukijua kuwa ana mke wake nyumbani. Kumuiba mume wa mtu sio tu kwamba ulimuumiza mwanamke mwenzio na watoto ambao wamezaliwa ndani ndoa yake bali unachangia kwa kiasi kikubwa kufanya watu wasiheshimu ndoa tena.


Familia yako haitaki kumsikia kabisa Mpenzi wako kwa vile wanajua kuwa ni mume wa mtu mwingine, wanakupenda na wasingependa na wewe kwenda kupata matatizo ambayo mke wa huyo jamaa anayapata kwa sababu yako. Yaani wanahofia kuwa Jamaa akikuoa atakuacha na kwenda kutafuta mwanamke mwingine kama alivyokuja kwako.


Huyu bwana ni mnafiki na muongo, kama mkewe kamtenga kwa miaka yote Mitano jiulize kwa nini basi hakumpa Talaka? Hiyo pekee inakuambia kuwa jamaa anampenda mke wake na hayuko tayari kumuacha kwa ajili yako. Hilo moja.


Kitu kingine cha wewe kuzingatia ili kugundua kuwa huyu bwana hana mpango na wewe kama mkewe ni kuwa, kwa kawaida mwanaume aliyetulia kiakili, kimaisha (sio mwanafunzi) hawezi kukaa na wewe kwa muda wa miaka mitano bila kutangaza ndoa.....mwisho ni mwaka mmoja tu....anataliki na kukuoa wewe(kama anamke) na ikiwa hakuwahi kuoa basi inakuwa kama vile kutereza mahali pakavu....pili.


Tatu, inakuwaje awe ametengwa na wanalale vitanda tofauti lakini kila siku anakwenda kulala kwa mkewe? Oh well, anaweza kuzuga tu ili jamii isigundue uchafu wake au wasihisi kuwa yeye na mkwewe wanauhusiano wa ajabu (huenda wameelewana hivyo kwa vile mkewe hawezi kumpa ngono ya kutosha mumewe).


Kama nilivyogusia hapo juu, kuna uwezekano mkubwa kabisa wameelewana kuwa Mume akutumie wewe tu(asibadili wanawake kila leo) kwa ngono kwa vile yeye mkewe hawezi kumpa ngono mumewe kama ambavyo anahitaji.


Sasa ili kukufanya usimuache na kuwa na mwanaume mwingine (kutokana na maelewano na mkewe) hali inayoweza kuwaweka kwenye hatari ya kuambukizwa VVU......anajitahidi kukupa huduma zote unazohitaji.......usijiamini nakusema alisalim amri kumbe wawili hao wanajua walifanyalo.


Usikute wanapendana sana na wanafanya mapenzi kila wanapohitajiana lakini kwa vile anajua wazi kabisa akikuambia wewe hivyo hutofurahi hivyo ni heri kukuambia kile unachotaka kusikia.....(wanaume wengi husema kile wanawake wanapenda kusikia ili kuepuka mizozo au kuachwa).


Hakuna wakati wa kuwa na mume wala muda wa kuolewa unless unataka kufunda ndoa kwa sababu nyingine na sio mapenzi. Umri wako ni mdogo sana kuhofia muda wa kuolewa (hiyo kuolewa b4 hujafikisha miaka 30 waachieni wenye kuamini kuolewa ni bahati).


Lakini wewe Olewa unapokuwa na mpenzi mmoja (sio mpenzi wa mtu) mnapendana kwa dhati,wote mnania moja ya kuishi maisha yenu yote pamoja na mko tayari kwa wakati huo. Vinginevyo furahia maisha yako kama yanavyokuja.


Nini cha kufanya-Maliza uhusiano na mume huyo wa mwenzio, kufanya hivyo sio mwisho wa maisha yako bali ni mwanzo mpya wa maisha yako. Bado kijana na ninauhakika kabisa utapata mpenzi mpya ambae atakuwa mume wako peke yako.


Tangu umekuwa na uhusiano na mume wa mtu umedai kuwa hakutokea hata mwanaume mmoja aliyekutamkia kuwa anakupenda hata kwa kinafiki, ni kwa vile walikuwa wanakuiba hivyo hakukuwa na sababu ya wao kuji-commite kwako wakati wanajua kwamwe huwezi kuwa wao peke yako........wanaume hawapendi kuchangia, wanapenda kumiliki mwanamke wake peke yake.


Hivyo ukiachana na huyo Mume wa watu, utaona watakavyo miminika. Jitahidi tu kubadilisha mtindo wa maisha yako (soma makala hapo chini).

Kila la kheri.

No comments:

Pages