Monday

Miaka 5 na mume wa mtu, Hamkunielewa-Ushauri.

"Nashukuru sana da dinah pamoja wachangiaji wote mlioniponda na kunipa ushauri mzuri katika mada yangu Miaka 5 na mume wa mtu!


Kifupi ni kwamba huyu bwana yuko tayari kumpa talaka mkewe ila mimi siko tayari kwahilo. Pili kuhusu kuolewa yuko tayari mda na siku yoyote hata leo ila dini zetu zinaleta pingamizi nami naliona gumu pia kwani siwezi kuwa muislam na yeye alishambadilisha mkewe dini na kumpeleka uislam hivo hawezi kuja ukristo amwache mkewe huko.


Naombeni tena mnisaidie nitumie mbinu gani nitumie katika kuachana na huyu bwana na ni mda gani muafaka wa kutumia katika kulizungumzia hili kwani kila nikijaribu kumtajia hilo tu ni ugomvi na inakuwa kama ndo nimemwambia ahamie kwangu kwani atalala kwangu mwezi mzima bila kwenda kwake.


Kunitambulisha ameshanitambulisha kwao ndugu,wazazi, mkewe, watoto wote wananijua na wamenikubali ila kwangu naona sio kitu hilo kwani siko kwenye nafsi zao hivo uenda ni unafiki au ni ukweli.


Nashukuru sana kwa watakaonisaidia kutatua hili na sio kuniponda.

Kazi na siku njema wote Asanteni. "


Jawabu: Pole kwa kukwazika. Wasomaji wangu ni wazi walipatwa na hasira kwa sababu wasingependa kitu kama hicho kiwatokee wao au hata wanawake wenzao kwa imani kuwa wanawake tunapaswa kushirikiana na sio kuharibiana ndoa.


Mume/mke wa mtu akikutokea mkatae akizidi kukufuata fuata basi nenda kamwambie mkewe hali itakayofanya mke huyo kuwa awear na tabia chafu ya mume/mke wake....hapo utakuwa umesaidia kuokoa ndoa yao, maisha ya watoto wao (ni vema watoto kukua ndani ya ndoa wakiw ana wazazi wote 2) na kuongeza amani kwenye nyumba yao.




Majibu ya wengi yaliegemea kutokana na maelezo yako ambayo sasa umegundua kuwa hayakuwa yamejitosheleza au hayakuwa wazi kwenye points muhimu ambazo ni hizi:-


1-Kumbe jamaa ni Muislamu hivyo anahaki kabisa ya kuoa mke wa pili kwa mujibu wa Imani yake as long as anauwezo na sababu ya msingi ya kufanya hivyo.



2-Wewe hauko na haukuwa tayari kufunga nae ndoa ya kiislamu(hutaki kubadili Dini), which tells me kuwa wazazi wako hawamkubali jamaa kwa vile Dini yake ni tofauti na sio kwa vile ni mume wa mtu.


3-Mkewe, watoto, ndugu na jamaa zake wamekukubali kama mke wa pili lakini wewe ndio unasita kutokana na Imani zenu za Dini kuwa tofauti.


Ungeweka wazi yote haya ingesaidia wasomaji wangu kukupa ushauri tofauti na walivyokushauri mwanzo.*********************************************

Nimefurahishwa na nia yako ya kutaka kutoka kwenye uhusiano huo kama ambavyo wengi walikushauri, kwani ukikubali kuolewa ni wazi kuwa utakuwa umechangia kwa kiasi fulani kuharibu maisha ya watoto ambao tayari wamezaliwa kama matunda ya ndoa hiyo(haijalishi kama dini inaruhusu au la) suala muhimu ni kutokuwa wabinafsi na kuwafikiria watoto hao na maisha yao ya baadae.

Nasema hivyo kwa vile, watoto hao siku zote watakuwa wakichukulia au kuamini kuwa wewe umechukua nafasi ya mama yao na maisha hayatakuwa the same kwao kitu ambacho wengi huwa tunajaribu kukiepuka.

Watoto hao watalazimika kukupa heshima ya uoga (kwa vile baba anataka iwe hivyo), lakini mioyoni mwao hautokuwepo kabisa (jaribu kujiweka wewe kwenye their shoes.....ungejisikiaje?).

Hawatokupa upendo sawa na ule walionao kwa mama yao mzazi, hawatokuthamini kama vile wanavyofanya kwa mama yao mzazi hali itakayokufanya utamani kuzaa watoto wako mwenywe kitu ambacho kitaongeza idadi ya watoto na hivyo maisha yanaweza kubadilika kwani huwezi kujua nini kitatokea in 10yrs time.


Kama hao watoto hawatopata matunzo muhimu labda baada ya mama yako kuachika na wakaamua kwenda kuishi na mama (watoto wengi huenda na mama, mama are the best, we have strong bonds na we love mamas) au kushindwa kuendelea na masomo baada ya baba yao (mungu apishe mbali) kuodoka Duniani lawama zote zitakuangukia wewe, labda usingeolewa na baba yao na kuongeza Idadi ya watoto maisha yangekuwa tofauti hata kama Mzee hayupo.....si unajua mambo ya urithi!


Kujitoa kwako kwenye uhusiano na mume wa mtu kutakuwa kumeokoa ndoa ya mwanamke mwenzio, kuokoa maisha ya baadae ya watoto waliozaliwa kwenye ndoa hiyo na pengine litakuwa fundisho kwa mwanaume huyo na hivyo itakuwa mwisho wa kuwa na kimada.


Kuna mchangiaji mmoja kagusia kuhama mji, hiyo ndio njia nzuri na ya pekee ambayo inaweza kuua uhusiano haraka na kukusaidia kuanza maisha upya mkoa/kijiji/kitongoji/mji mwingine. Wakati unaendelea na mipango yako ya kuhama "nchi" humuambii mtu, ukikamilisha wewe unatoweka tu lakini julisha ndungu zako na hakikisha hawamuambii jamaa uko wapi.



Ili basi kumsaidia huyo jamaa, muandikie walaka wa kwanini umeamua kuua uhusiano wenu (usiseme unahamia wapi) na weka points muhimu wazi, Points muhimu ni kuhusu ndoa yake(onyesha kuwa hauko tayari kuharibu ndoa ya mwanamke mwenzio, usigusie suala la utofauti wa dini zenu), watoto na maisha yao ya baade(onyesha unajali maisha ya watoto hao kama vile ambavyo ungejali maisha yako wewe ulipokuwa mtoto).


Mungu atakubariki kwa kuokoa ndoa ya mwenzio na vilevile atakujaalia na utakutana na kijana kama wewe, mwenye nia moja kuwa na wewe kama mke wake.

Sio mwisho wa maisha kum-buti mpenzi, bali ni mwanzo wa maisha yako mapya.

Kila la kheri!

No comments:

Pages